Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shamsa asimulia walivyokutana na Mlilo hadi ndoa

Shamsaford 1692966077084.jpeg Shamsa asimulia walivyokutana na Mlilo hadi ndoa

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo kutoka kiwanda cha sanaa Bongo, Shamsa Ford amesema yeye na mumewe Mlilo, kabla ya kufunga ndoa walikutana kwenye kazi za uigizaji.

Akisimulia tukio hilo, Shamsa alisema walibadilishana namba na wakaja kuwasiliana baada ya kuonana tena kama miezi minne ilipita ndipo wakawa marafiki wa kawaida kabla ya kuingia kwenye mahusiano.

"Tulibadilishana namba akawa zile ananitumia ujumbe leo najibu baada ya wiki, lakini tulikutana tena baada ya kama miezi minne hivi ndipo sasa tukawa marafiki.

"Akawa ananielezea matatizo yake ya kwenye mahusiano na mimi namuelezea yangu hivyo basi tukajikuta tupo kwenye mahusiano na baadaye akanioa baada ya kuachana na mkewe aliyekuwa naye kabla yangu," alisema Shamsa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live