Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shamsa akanusha kuvunja ndoa ya mwanamke mwenziye

Shamsa Na Mlilo.jpeg Shamsa akanusha kuvunja ndoa ya mwanamke mwenziye

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amesema, hakuvunja ndoa ya aliyekuwa mke wa mumewe Mlilo kama ambavyo baadhi ya watu waliamini kutokana na uvumi uliotawanywa.

Shamsa ametoa kauli hiyo akiwa fungate na mumewe kwenye moja ya hoteli zilizopo jijini Dar baada ya kufunga ndoa hivi karibuni.

"Sikuvunja ndoa ya mtu, ni kweli nilifahamiana na mume wangu akiwa bado na mke mwingine na hata matatizo yao yalipokuwa yanatokea, mimi nilikuwa namshauri mwanamke mwenzangu cha kufanya na wakati huo sikuwa na mahusiano na Mlilo," alisema.

Shamsa amesema, walipoingia kwenye mahusiano alijua bado anaweza kuwa mke wa pili hivyo alikubali lakini mumewe alimpa talaka mwanamke mwenziye kwa kuwa walishindwana kwa mambo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live