Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shakira atuhumiwa kwa uhalifu wa kodi kwa mara ya pili

Shakira Atuhumiwa Kwa Uhalifu Wa Kodi Kwa Mara Ya Pili Shakira atuhumiwa kwa uhalifu wa kodi kwa mara ya pili

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Shakira alishinda tuzo ya mafanikio ya maisha katika Tuzo za Muziki za Video za MTV mapema mwezi huu

Mwanamuziki wa pop wa Colombia, Shakira amefunguliwa mashtaka ya kukwepa kulipa kodi kwa mara ya pili na serikali ya Uhispania.

Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanadai muimbaji huyo aliilaghai serikali ya Euro milioni 6.7 ($7.1m, £5.8m) mwaka wa 2018.

Wanasema hii ilitokea aliposhindwa kutangaza mamilioni ya malipo ya awali aliyopewa katika Ziara yake ya Dunia ya El Dorado, miongoni mwa malipo mengine.

Waendesha mashtaka wa Uhispania walianza uchunguzi wa pili mnamo Julai 2023, lakini walitoa maelezo Jumanne wiki hii.

Mtandao wa Kihispania wa RTVE unasema muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 46 anafahamu mashtaka mapya, lakini shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa timu ya wanasheria ya Shakira huko Miami - anakoishi sasa - bado haijaambiwa kuyahusu.

Badala yake, "walilenga kujiandaa kwa kesi ya miaka ya fedha ya 2012-14, ambayo itaanza Novemba 20," waliliambia shirika la habari la Reuters katika taarifa.

Mashtaka mapya yanatokana na ukweli kwamba mnamo 2018, Shakira alikuwa akiishi Barcelona na nyota wa mpira wa miguu Gerard Pique na kwa hivyo alitakiwa kutoa kodi ya mapato yake yote ya kimataifa alipokuwa huko.

Shakira anakabiliwa na kesi ya uhalifu sita kuhusiana na kodi mjini Barcelona mwezi huu wa Novemba - mashtaka ambayo ameyakanusha.

Chanzo: Bbc