Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shakira alirejea kwenye ndoa kupunguza stress

Shakira And Gerard Pique Shakira alirejea kwenye ndoa kupunguza stress

Thu, 24 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Kibao Cha Waka Waka, Shakira amefunguka kuwa aliamua kurudi kufanya muziki Ili kuepukana na huzuni iliyokuwa ikimkabiri baada ya kuvunjika Kwa uhusiano wake na Gerard Pique waliyedumu naye Kwa zaidi ya muongo mmoja.

Shakira amefunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano na jarida la GQ Spain, ambapo alieleza kuwa alikaa kimya kwa miezi kadhaa baada ya tukio hilo lakini, hakuweza kuanza kupona mpaka ndipo alipoamua kuandika muziki tena.

Pia aliongeza kuwa ilikuwa vigumu kutambua udhaifu wake wote na kuwaweka wazi kwa ulimwengu kusikia lakini, imemsaidia kuanza mchakato wa uponyaji na kurudi tena katika hali yake ya kawaida baada ya kufanya tena muziki.

Shakira na Gerard walitangaza kuvunjika kwa uhusiano wao mnamo Juni 2022 baada ya zaidi ya muongo mmoja wa kuwa pamoja, ambapo ripoti za usaliti zikimuandama zaidi Gerard Pique, huku Shakira amekana kuwa sababu ya kuvunjika Kwa uhusiano wao.

Shakira ametoka hadharani mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni kuzungumzia uhusiano wake wa mapenzi na Gerard Pique, akisema aliweka kazi yake pembeni kwa ajili yake, na kuongeza kuwa kuwa na mume kulimrudisha nyuma kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live