Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shakira alipa faini ya Tsh bil 20 kukwepa kutupwa jela

Shakira Afikia Makubaliano Kuhusu Kesi Ya Ulaghai Wa Kodi Uhispania Shakira alipa faini ya Tsh bil 20 kukwepa kutupwa jela

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Muziki wa Pop na Raia wa #Colombia, #Shakira amefikia makubaliano na Waendesha Mashtaka wa kumaliza Shauri la kukwepa Kodi kwa kulipa Euro Milioni 7.5 (Tsh. Bilioni 20.4) kabla kesi ya msingi haijaanza kisikilizwa.

Awali, Shakira alitakiwa achague kulipa kiwango hicho ili mambo yaishe au Shauri liende Mahakamani na akishindwa kesi kuna kifungo cha Miaka 8 jela na Faini ya Euro 23.8m (Tsh. Bilioni 65), akachagua Mahakamani kabla ya kubadili mawazo baadaye.

Shauri la Msingi lilikuwa kukwepa Kodi ya Euro Milioni 14.5 (Tsh. Bilioni 39.4) lililowasilishwa Mahakama ya Barcelona

Chanzo: www.tanzaniaweb.live