Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shakira afikia makubaliano kesi ya ulaghai wa kodi Uhispania

Shakira Afikia Makubaliano Kuhusu Kesi Ya Ulaghai Wa Kodi Uhispania Shakira afikia makubaliano kesi ya ulaghai wa kodi Uhispania

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Nyota wa muziki kutoka Colombia, Shakira amefikia makubaliano na waendesha mashtaka wa Uhispania kutatua kesi ya ulaghai wa kodi, wakati kesi yake ilipokaribia kuanza.

Mwimbaji huyo wa Hips Don't Lie alikabiliwa na madai ya ulaghai wa kodi ya kiasi cha €14.5m (£12.9m) katika mahakama ya Barcelona.

Waendesha mashtaka wa Uhispania walitaka kumfunga jela miaka minane na kumtoza faini ya euro milioni 23.8 ikiwa angepatikana na hatia.

Shakira, ambaye mara kwa mara amekanusha makosa yoyote, aliamua kuafikiana na uoande wa mashtaka "kwa maslahi ya watoto wangu moyoni".

Aliongeza "hawataki kuona mama yao akisalimisha ustawi wake wa kibinafsi katika vita hivi".

Msanii huyo hapo awali alikataa mpango uliotolewa na waendesha mashtaka, badala yake akachagua kwenda mahakamani.

Chanzo: Bbc