Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Shakira aacha kazi kisa penzi la Gerrard Pique

Shakira X Pique Shakira aacha kazi kisa penzi la Gerrard Pique

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akiongea kwenye mahojiano mwishoni mwa wiki mwanamuziki wa colombia Shakira amedai kuwa kazi yake ya muziki aliipa kipaumbele cha mwisho kwa miaka mingi kwa sababu ya mpenzi wake wa zamani Gerard Piqué (mchezaji wa zamani wa Barcelona).

Shakira ambaye kwasasa ana umri wa miaka 47 anasema...."Kwa muda mrefu nilisimamisha kazi yangu ili kuwa karibu na Gerard, ili aweze kucheza mpira........kulikuwa na kujitolea kwingi kwa ajili ya upendo" aliongeza.

Nyota huyo wa muziki wa Colombia na mchezaji kandanda wa zamani wa Uhispania walikuwa pamoja kwa miaka 11 kabla ya kuachana Juni 2022.

Mastaa hawa wana watoto wawili Milan na Sasha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live