Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Shakilla: Mahari yangu Sh milioni 265

Shakila Mweh Shakilla atangaza mahari yake

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasosholaiti Shakilla ameweka wazi bei ya mahari yake kwa yule aliye na nia ya kumwoa.

Kwenye mtandao wa Instagram, Shakilla alisema kuwa mahari yake itakuwa Ksh milioni 15 (sawa na tsh milioni 265) pamoja na ngamia wapatao 100. Aliongeza kuwa lazima pia uwe na vocha ya Ksh 520,000 (sawa na tsh milioni 9.18).

Pamoja na hayo, Shakilla alisema atapewa nyumba kwa jina lake na gari la Range Rover. Pia anasema mwenye atamuoa atamlipa marupurupu ya Ksh 195,000 (sawa na Tsh 3.45) kila mwezi.

Katika wakati wa maswali, shabiki mmoja alimuuliza kama anaweza kumpeleka kwenye 'lunch date'. Shakilla alijibu..." iwapo unataka kunipeleka kwenye 'date' lazima unipe Ksh 13,000 (Tsh 230) na dereva wa kibinafsi".

Shakilla alisema atakayempleka amlipie vyakula na vipodozi vyake na awe na simu isiyo chini ya iPhone Promax, lazima awe mpiga picha bora na awe na uwezo wa kumpeleka kwenye hoteli ya 5 star.

Shakilla mwenye miaka 20, amekuwa gumzo mitaani haswa baada ya kudai kwamba hakika hayuko sawa kutokana na kuburuzwa vikali mitandaoni.

Baada ya kubainisha kwamba alikuwa na uchu wa kuigiza filamu za watu wazima, baadae mwanasosholaiti huyo aliibuka tena miezi michache iliyopita akionesha wasiwasi wake kuwa hakuna mwanamume aliyetaka kuchumbiana na yeye, akihisi kwamba pengine alizaliwa kuwa mtu wa mitaani tu na wala si mke wa ndoa.

“Kwa hiyo tuseme katika wanaume wote ambao wananifuata Instagram hakuna hata mmoja anayetaka kuingia katika uhusiano wa hakika na mimi. Kwani mimi nilikusudiwa kuwa wa mitaani katika maisha yangu yote bila familia?” Mwanasosholaiti huyo aliuliza kwa wasiwasi mkubwa.

Umaarufu wa mwanasosholaiti huyo ulikua kwa kasi mwaka 2020 wakati wa janga la Covid-19 alipotambulishwa na Xtian Dela kwenye kipindi kilichonuia kuwawezesha wasanii kutumia muda wao vizuri wakati huo ambao shughuli nyingi zilisimama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live