Kuna video inatrend mitandao ya Kenya na Tanzania ikimuonesha msanii @iamlavalava amelala na mwanamitandao Shakilla Tiffany @i.am_shakilla akijirekodi video wakiwa wote kitandani.
Shakila ametolea maelezo video hiyo akisema ameshangazwa kuiona, hausiki nayo kusambaza pia ni video iliyorekodiwa miaka miwili iliyopita.
"Kuna video inazunguka "Online" mimi na aliyetajwa kwenye video. Ningependa ijulikane kuwa nimeshangazwa kuiona. Hiyo video imechukuliwa miaka miwili iliyopita kwenye simu ya mtu mwingine ambaye sijazungumza au kumuona kwa zaidi ya mwaka".
"Siwezi kurudi nyuma wala kujibu maswali kuhusu hiyo video. Sihusiki/siwajibiki kwa kupost video kupata engagements kwa huyo mtu" ameandika kupitia Insta Story yake.