Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shah Rukh Khan apewa heshima ya kipekee Dubai

Shah Rukh Khan Shah Rukh Khan apewa heshima ya kipekee Dubai

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mnamo mwaka 2016, Shah Rukh Khan aliteuliwa Brand Ambassador wa Dubai na Idara ya Utalii na Biashara (DTCM).

Ushirikiano huu ulilenga kuimarisha sifa ya kimataifa ya Dubai na kutangaza jiji hilo kama kivutio kikuu cha utalii, biashara na burudani Duniani.

Mnamo Mwaka 2022 Ushirikiano Huu ulifikia kikomo. Lakini Ushirikiano Huu ulimfanya Shah Rukh Khan Kuwa Ndio Mtu Maarufu Wa Kwanza Kupata UAE Golden Visa.

Ukiwa Na UAE Golden Visa Inakupa Nafasi ya Kuweza Kufanya Vitu Vingi Ukiwa Ndani Kama Kuweza kukaa/ Kuishi Muda Mrefu Bila Ku renew visa, huhitaji "Sponsor" Pale Unapotafuta Kazi, kupitia Golden Visa Hiyo Unaweza kuwadhamini family members Wengine, Unakuwa Na Idadi isiyo Na kikomo kuwadhamini Watu wanaohitaji Kufanya Kazi, Kama Holder Wa Golden Visa Akifariki, family members Wengine wanaruhusiwa Kuendelea Kuishi Kuitumia visa Hiyo hiyo Mpaka itakapoisha Muda wake.

Dubai, yenye anga ya kuvutia, hoteli za kifahari, na miundombinu ya hali ya juu duniani, inayowiana kikamilifu na ukubwa wa Shah Rukh Khan kwa namna anavyotambuliwa kimataifa. Umaarufu wake mkubwa,Charisma aliyonayo na idadi kubwa ya mashabiki ilimfanya kuwa chaguo bora la kuwakilisha taswira ya Dubai yenye kuvutia kimataifa.

Pamoja Na kwamba Ushirikiano Na DTCM ulikoma 2022, Shah Rukh Khan Ameweza Kupata Nafasi Nyingine Kama face of regional healthcare operator Burjeel Holdings, Ambayo inamiliki hospital 39 UAE Pamoja Na Oman . Na Kwa Nafasi Hii imemfanya Shah Rukh Khan Kuweka kibindoni US Dollar Million 4 {USD $ 4m}.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live