Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shah Rukh Khan: Ndani ya miaka 28 nimefanya sajari 11

Shah Rukh Khan H.jpeg Shah Rukh Khan.

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shah Rukh Khan (58) anasema ndani ya miaka 28 sasa alishafanyiwa sajari 11 mwilini mwake ambazo zimetokana na kuumia wakati akishuti filamu mbalimbali, miongoni mwa sajari alizofanyiwa ni ya goti, bega na pua.

Aliumia alipokuwa akishuti filamu zikiwemo Darr, Koyla, Raees, My Name Is Khan, Happy New Year, Chennai Express, Ra.One.

Siku nne baada ya kuanza kushuti filamu ya Kal Ho Naa Ho(2003) Shah Rukh Khan alianza kuumwa na mgongo, aliwaeleza waandaaji wa filamu husika kuwa nafasi yake wanaweza kumpa mwigizaji mwingine kwani maumivu ya mgongo yalikuwa makali.

Hata hivyo, wandaaji waliamua kuaahirisha shutingi kwa kuisogeza mbele ambapo miezi sita baadaye alipotibiwa na kuwa sawa ndio wakaendelea na uchukuaji wa picha za filamu husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live