Zaidi ya mashabiki wapatao 60,000 waijaza show ya Beyoncé katika jijila Cardiff nchini Wales kushuhudia onyesho la uzunduzi wa tamasha la dunia muziki wake analotarajia kulifanya katika maeneo mbali mbali duniani.
Watu walisafiri kutoka maeneo mbali mbali duniani kumuona muimbaji huyo akiwa jukwani katika Uwanja wa Principality.
Walitoka maeneo ya mbali kama vile Marekani, Lebanon na Australia na walikuwa wameanza kupanga misururu saa 12 kabla ya onyesho kuanza Jumatano.
Mmoja wa mashabiki alisema anamkubali sana Beyonce na hata angefurahi “iwapo angenipaka jasho lake”.
Tamasha la Renaissance World Tour ni la kwanza kufanywa na Beyoncé mwenye umri wa miaka 41-year-katika kipindi cha miaka saba.
George Crocker, 15, ambaye alikuja kutoka Avoca Beach, New South Wales, Australia, alisema: “Ninashukuru sana kupata fursa hii na nimekuja, hatimaye nimemuona Malikia Beyonce.
“Ni muungu wa kike, ni mama yangu. Ni malkia kabisa…ni kila kitu katika mtu. Kila kitu kumuhusu ni kamili.”
George Crocker, 15, alisafiri kutoka Avoca Beach nchini Australia na mama yake kushuhudia tamasha.