Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Shabiki Man United ala mayai 15, akimbizwa hospitali

Mayai Ety.jpeg Shabiki Man United ala mayai 15, akimbizwa hospitali

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki wa Manchester United, Thomas Kiptanui Kemboi maarufu Kapkeno aliwahishwa hospitali nchini Kenya baada ya kula mayai 15 ya kuchemsha aliyobeti na shabiki mwenzake wa Arsenal kuwa endapo wangefungwa angekula trei zima.

Arsenal ilicheza na Manchester United wikiendi iliyopita na kushinda mabao 3-1, Kapkeno anayeishi Eldoret ndiye aliyejihakikishia kuwa atakula trei zima la mayai kama Arsenal itaifunga Man U na alitimiza kwa kula mayai hayo akipumzika kwa kunywa maji.

Alipofikia yai la 15 alipoanguka ghafla na wenzake kuhisi utani ila hali ilipobadilika walimpeleka haraka hospitali na alibainika kuwa na tatizo la kukosa kupata choo ambapo alilazwa na kuruhiswa baada ya hali kukaa sawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live