Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seth kuzikwa Jumatatu, familia yaomba msaada

87541 Pic+kuzikwa Seth kuzikwa Jumatatu, familia yaomba msaada

Sat, 7 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Familia ya marehemu Seth Bosco ameamua itamzika msanii huyo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania Jumatatu ya Desemba 9, 2019.

Hayo yamesema leo Jumamosi Desemba 7, 2019 na msemaji wa familia, Novatus Mayenja maarufu kwa jina la Nova alipokuwa akitoa matangazo ya ratiba za msiba huyo, uliopo Kimara Temboni, Dar es Salaam.

"Kama familia, tumekaa kikao na mwisho wa siku tumeamua ndugu yetu tutamzika hapahapa Dar es Salaam, siku ya Jumatatu Desemba 9,2019," amesema

Gharama zitakazotumika katika mazishi yake ni Sh10 milioni ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali katika mazishi.

Shughuli hizo ni pamoja na kununua jeneza, kukodi usafiri wa kubeba mwili, maturubai, viti, kununua vyakula vya kupika kwa ndugu jamaa na marafiki watakaofika nyumbani na kipindi chote cha msiba.

"Gharama hizi kama hivyo mnaziona ni kubwa familia peke yake haitaweza kuzibeba, tunaomba watu mbalimbali mjitokeze kuchangia chochote mlichojaliwa ili tuweze kumpuzisha ndugu yetu kwenye nyumba yake ya milele," amesema Nova.

Seth ambaye ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba amefikwa na mauti usiku wa kumakia leo Jumamosi Desemba 7, 2019 jijini Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz