Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Serikali yapiga marufuku mtandao wa TikTok

Tiktok.jpeg Serikali yapiga marufuku mtandao wa TikTok

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Ulaya imepiga marufuku wafanyakazi wa Umoja wa Ulaya (EU) kutumia mtandao wa TikTok.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia Marekani na serikali za Magharibi kupiga marufuku matumizi ya mtandao huo unaomilikiwa na China kwa sababu za kiusalama, kufuatia uhusiano mbaya na Beijing.

Wafanyakazi wameamriwa kufuta programu tumizi hiyo kwenye vifaa vya kazi, lakini pia kuiondoa kwenye vifaa vyovyote binafsi vyenye programu zinazohusiana na kazi ama la, wafute programu zinazohusiana na kazi ikiwa wanataka kubakiza TikTok.

Tume imewapa wafanyakazi hadi Machi 15 mwaka huu kufanya hivyo ili kulinda taarifa na kuimarisha usalama wa mtandao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live