Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yampongeza Miss Tanzania

479ac561e861d10336f258713d2c9d97.png Serikali yampongeza Miss Tanzania

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSHINDI wa taji la Urembo wa Tanzania (Miss Tanzania) 2020, Rose Manfere ametakiwa kutumia urembo wake kuitangaza nchi vizuri.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashugwa, alipokutana na mrembo huyo na kusema serikali itaendelea kumpa ushirikiano katika kutekeleza wajibu wake kwa Taifa kwa amebeba dhamana ya kutangaza nchi.

“Serikali tutakuunga mkono katika jukumu la kupeperusha bendera ya nchi katika tasnia ya urembo, tumia fursa hii kutangaza utamaduni wetu, mila na desturi za taifa letu na zaidi utalii unaopatikana hapa nchini,” alisema Bashungwa.

Aidha Bashungwa amempongeza mratibu wa shindano hilo, Basila Mwanukuzi kwa kuendesha shindano hilo kwa weledi kwani yamefanikisha kupatikana kwa mwakilishi wa kutangaza nchi na katika mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2021.

Naye Basila Mwanukuzi aliishukuru serikali kwa kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha shindano hilo na kuahidi kuwa mrembo huyo atafanya vizuri katika mashindano ya dunia.

“Watanzania naomba tutoe ushirikiano kwa mrembo huyu kwani akifanikiwa nchi pia imefanikiwa hivyo tumuunge mkono,” alisema Basila.

Chanzo: habarileo.co.tz