Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafunguka Rayvanny kufanya show tuzo za MTV EMA

RAYVANEMMA Serikali yafunguka Rayvanny kufanya show tuzo za MTV EMA

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: Habarileo

Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, imempongeza msanii ‘Rayvanny’ kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania, kutumbuiza katika usiku wa tuzo za MTV EMA zilozofanyika Budapest nchini Hungary.

“Tunampongeza msanii Rayvanny kwa kuwa msanii wa kwanza kutumbuiza katika tuzo za MTV EMA,”ilieleza taarifa ya wizara kupitia Instagram.

Aidha wasanii mbalimbali nchini wamempongeza msanii huyo kwa hatua hiyo. Diamond Platnumz ni miongoni mwa waliotoa pongezi hizo na kushauri vijana namna nzuri ya kufanikiwa.

“Vijana wenzangu tujifunze, kuwa na nidhamu na fadhila ili sanaa zetu zitufikishe mbali zaidi,”ameandika Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: Habarileo