Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaahidi uboreshaji studio za THT

THT HQ Serikali yaahidi uboreshaji studio za THT

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi ametembelea kituo cha Sanaa na Ubunifu cha Tanzania House of Talents (THT) Mikocheni DSM kilichoasisiwa na Marehemu Ruge Mutahaba na kuahidi maboresho.

Katika kuunga mkono kituo hicho, Dk Abbasi ameahidi kuchangia uboreshaji wa studio pamoja na kuiunganisha THT na Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ili washirikiane kuendeleza vipaji vya vijana Tanzania.

"Sisi wanadamu ndio tunafika mwisho lakini siku zote ndoto kuu hazifi, niko hapa leo kuwaahidi kuwa mimi na wenzangu wengine wengi nitakaowakusanya wakiwemo Wasanii waliopita hapa THT tutashirikiana kuiendeleza THT,” alisema Dk Abbasi

Mkurugenzi wa sasa wa THT, Kemi Mutahaba amesema ili kuiongezea thamani ya mafunzo THT, wanatarajia kuandaa mtaala na utoaji vyeti kwa Vijana

Chanzo: habarileo.co.tz