Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kumwaga tena mikopo kwa wasanii

9eba1d8d Ec81 4090 Ab65 D097008c6169 Serikali kumwaga tena mikopo kwa wasanii

Fri, 27 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dokta Hassani Abbas wametembelea ofisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa jijini Dar es Salaam na kufanya kikao kazi na watumishi wa mfuko huo.

Mchengerwa amefafanua kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria na imeanza kuwezesha wasanii kimitaji ili kuboresha maisha yao.

Aidha,  amesema  wiki ijayo Serikali itatoa mikopo ya awamu ya pili  baada ya ile ya mwanzo iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana.

Ameongeza kuwa katika tukio hilo pia Serikali itapokea mdundo wa taifa na vazi la Taifa kutoka kwenye Kamati za kitaifa alizoziteua kufanya kazi hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live