Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuanza kutoa mikopo nafuu kwa wasanii

91ce9ae415ca83fa89b96e1bd863ef9d Serikali kuanza kutoa mikopo nafuu kwa wasanii

Wed, 12 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ili kuwasaidia wasanii kupata mitaji kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu kuanzia Julai mwaka huu.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Hassan Abbasi, amesema jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa tamthilika ya ‘We Men’ itakayorushwa na kituo cha Star Times.

“Tayari mfuko huo wa wasanii umepangiwa bajeti yake na kuanzia mwaka huu wa fedha unaoanza Julai , wasanii mtaweza kunufaika nao ikiwemo kupata mikopo ya kuboresha kazi zenu na kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.” alisema na kuongeza

“Hivyo ni wakati sasa wa wasanii kuwa karibu na vyama vyenu na taasisi zinazowasimamia wakiwemo Basata, Cosota na Bodi ya filamu, ambao hawa watahusika kwa karibu katika kuratibu suala hili.” alisema.

Katibu huyo amesema kurejesha mfuko huo kutaondoa malalamiko ya wasanii wengi ambao wanadai wanakuwa na wazo lakini wanashindwa kuliwazua kutokana na ukosefu wa fedha.

Mfuko huo ulianzishwa Novemba 2019 katika kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere lililofanyika mkoani Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu siku hiyo aliuchangia Shilingi milioni tano huku Hayati John Magufuli aliahidi kuuchangia Shilingi milioni 100 katika uanzishwaji wake.

Aidha alisema serikali imepanga kufanya mapinduzi makubwa katika sanaa na kuwataka wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ambazo zitapenya kwenye soko la kimataifa.

“Sio mnatengeneza filamu jambazi anaenda kupora amevua viatu, tumeshatoka huko,” alisema

Katika hatua nyingine Meneja masoko StarTimes, David Malisa, amesema wamejipanga katika kukuza kazi za Sanaa hapa nchini, ambapo kwa mwaka 2020 katika kampuni hiyo jumla ya filamu 104 zimeonyeshwa huku shilingi milioni 280 zikiwa zimewekezwa kwa shughuli hiyo.

Kwa pande wake Max Rioba ambaye ni muandaaji wa tamthilia ya ‘We Men’, alisema wamejitahidi kuiandaa filamu hiyo katika kiwango cha kimataifa na wanaamini italeta mapindusi katika tasnia ya filamu kwa ujumla.

Wasanii waliopo katika filamu hiyo ni pamoja na Max mwenyewe, Wema Sepetu, Shilole, Hemed Suleiman na Grace Mgonjo ambaye ni mke wa Profesa Jay.

Chanzo: www.habarileo.co.tz