Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali idhiditi wadukuzi wa kazi za sanaa - Batuli

BATULI MSZ Batuli

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ina deni la kuhakikisha inaweka mfumo bora wa kudhibiti wadukuzi wa kazi za sanaa ili kuwahusika wa kazi hizo waweze kufaidika lakini kutopoteza mapato.

Kauli hiyo imetolewa na mwigizaji mkubwa wa filamu nchini, Yobnesh Yusuph maarufu 'Batuli' alipozugumza nasi kuhusu mwenendo wa kiwanda cha filamu nchini.

Akizungumza leo Juni 4, 2024 na mwandishi wa mtandao huu, Batuli ambaye kwa sasa ana miaka 24 katika sanaa hiyo amesema endapo serikali itadhibiti biashara hiyo haramu itaongeza mauzo halisi na halali kupitia kazi zao, lakini pia serikali iwasaidie kusaka masoko ya nje.

"Bahati mbaya viongozi husika wamekuwa wakibadilishwa mara kwa mara naamini isingekuwa mabadiliko ya uongozi kwa mtindo huo tungefika mbali sana, tulianza kuyaona wakati wa Mheshimiwa Nnape Nauye na pia kwa Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa, nakiri walitusogeza pakubwa sana," amesema Batuli.

Batuli ametaja changamoto zinazowakabili waigizaji kuwa ni uwepo wa malipo madogo tofauti na ukubwa wa kazi wanazofanya, ambapo mwigizaji akikataa kutokana na hilo, mwingine anakubali amesema hali hiyo inashusha thamani ya kazi yao.

"Changamoto nyingine ni kutokuwa na sheria na kanuni sahihi za kuigiza waigizaji wapya hawapitii madarasa ambayo sisi tulipitia, wengi wao wanatoka waliopotoka na umaarufu wa vituko vyao vya hovyo, mitandaoni kisha wanajazwa kwenye uigizaji matokeo yake ni kuwa na waigizaji wenye skendo chafu na vituko vya ajabu," ameeleza Batuli.

Batuli amesema kwa hali hiyo wakati mwingine inakuwa ngumu mzazi kumruhusu mtoto ambaye ana kipaji na elimu ya sanaa ya uigizaji kuingia kwenye kazi hiyo.

Pia, amegusia suala la mazingira ya kufanyia kazi zao, ambapo amesema hakuna maeneo maalum yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya kazi zao za uigizaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live