Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Serengeti yashinda tuzo ya Hifadhi Bora Afrika

50ba6823029908044fec061e64661cd1 Serengeti yashinda tuzo ya Hifadhi Bora Afrika

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MBUGA ya Wanyama ya Serengeti iliyopo nchini Tanzania imeshinda Tuzo ya Hifadhi Bora katika Bara zima la Afrika kwa mwaka 2021 ambapo hii inakuwa ni mara ya tatu mfululizo Hifadhi ya Serengeti inashinda Tuzo hiyo.

Serengeti ilikuwa ikichuana na Mbuga nyingne ikiwemo Kalahari Games Reserve (Botswana), Etosha (Namibia), Kidepo Valley (Uganda), Kruger (Afrika Kusini) na Masai Mara ya Kenya.

Tuzo hizo zimetangazwa na World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani ambapo mwaka 2019 na mwaka jana 2020 pia Serengeti ilishinda Kundi la Hifadhi zinazoongoza kwa ubora Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz