Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senga ataka akifa azikwe na shuka la Yanga

SENGA+PIC Senga ataka akifa azikwe na shuka la Yanga

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By OLIPA ASSAMSANII wa vichekesho nchini, Ulimboka Mwalulesa maarufu kama Senga, ametoa kali ya mwaka kwamba siku akiondoka duniani azikiwe na shuka la Yanga, timu ambayo anaishabikia.

Senga amesema hata Yanga, ingefungwa kiasi gani hawezi kuihama atakomaa nayo mpaka kieleweka kwani anajua ipo kwenye mpito na itakaa sawa.

"Yaani hata nikifa nitazikwa na shuka la Yanga kwani nimeipenda mwenyewe hakuna aliyenilazimisha kuipenda, kwasababu ni timu ambayo inafanya maajabu,"amesema.

Aliigeukia Simba ambayo ni bingwa wa nchi wa Ligi Kuu Bara kwamba inatamba kwenye ligi hiyo, lakini itakapokutana na Waarabu itakuwa inafungashiwa mabao kama imetoka sokoni kununua machungwa.

"Yaani Simba inavyotamba itakomeshwa na Waarabu, wataanza kutia huruma utadhani imetoka sokoni kununua machungwa, watapigwa tano, sita, hivyo siumii na wanavyotamba kwani tunasubiri muda ambao wao watalia,"amesema.

AMTAJA MAGUFULI KUWA SHUJAA

Chanzo: mwanaspoti.co.tz