Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Selengo: Nicole kichwa, lakini...

Nicole Berry Selengo: Nicole kichwa, lakini...

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na mtayarishaji wa sanaa ya vichekesho, Abdul Mohamed a.k.a Ben Branco na maarufu zaidi kama 'Selengo' amefunguka ugumu wa kufanya kazi na Nicole Joeberry.

Akizungumza na Mwanaspoti, Selengo amesema licha ya kuwa msanii, pia ni mtayarishaji na amefanya kazi na staa huyo anayefanya vizuri kwenye Tamthilia ya Huba.

"Kufanya kazi na Nicole inahitaji moyo kwani licha ya kuwa na uelewa mkubwa lakini ni mtu ambaye anadeka sana kazi ya kufanya saa mbili mnaweza mkamaliza kwa saa tano hadi sita," amesema.

"Kazi ya Huba ili kuweza kuigiza unatumia script, hivyo unahitajika kuwa na uharaka wa kusoma au kukariri mambo ili uweze kurekodiwa kwa usahihi, basi bwana nilipewa kazi ya kumshuti Nicole," amesema.

Selengo amesema licha ya kufanya naye kazi kwenye Tamthilia ya Huba, yeye alianza kwa kumshuti kabla ya kuigiza naye pamoja, changamoto kubwa ni madeko.

"Ni msanii ambaye anajua sana na ana kichwa chepesi cha kukariri mambo, lakini shida yake hapelekeshwi, anafanya anavyojisikia yeye, hawezi kwenda na muda."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live