Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Selena Gomez amemtumia Rema kurudisha umaarufu - Steve Stoute

Selena Na Rema.jpeg Selena Gomez amemtumia Rema kurudisha umaarufu - Steve Stoute

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara na CEO wa ‘UnitedMasters’ Steve Stoute kutoka nchini Marekani amedai kuwa mwanamuziki Selena Gomez alimtumia mkali wa Afrobeat Rema kurudisha umaarufu wake.

Wakati akiwa kwenye mahojiano na Podcast ya ‘Afrobeats Intelligence’ aliweka wazi kuwa mwanamuziki huyo kutoka Marekani aliutumia wimbo wa ‘Calm Down’ ambao alishirikishwa na Rema kurudi katika game ya muziki, huku akidai kuwa haikuwa na ulazima kutoa remix ya wimbo huo kutokana na wenyewe kuwa mkubwa.

Remix ya ‘Calm Down’ iliachiwa rasmi mwaka mmoja uliopita, ambapo mpaka kufikia sasa inazaidi ya watazamaji milioni 794 kupitia mtandao wa #Youtube, ambao pia ulifanikiwa kuchukua tuzo ya MTV katika kipengele cha ‘Best Afrobeat song’. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live