Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Selemani' ya Mbosso ni bonge la wimbo

Mbosso: Napenda Kuigiza, Nipeni Dili Mbosso Khan

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wimbo Selemani wake Mbosso ni moja kati ya nyimbo wenye ujumbe nzuri na wakuelimisha ambao unafanya vizuri kwa sasa kwenye kila redio, runinga pamoja na mitaani.

Ni nyimbo chache za kuelimisha ambazo zinaweza kukubalika na jamii kwa urahisi hali ambayo imekuwa ikiwaogopesha wasanii wengi kutoa ngoma na kuelimisha na kujikita kwenye bata na mapenzi.

Ishara ya mafanikio ya ngoma kama hizi ni nzuri, ingawa wadau wengi wa burudani wakiwemo wasanii wamekuwa wakiamini ngoma za namna hiyo haziwezi kupenya.

Mbosso amekuwa akikutana na shangwe kubwa kupitia wimbo huo hali ambayo inatafsiriwa ni mafanikio katika macho ya wengi ambao hawaamini kwenye nyimbo zakuelimisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live