Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Selemani: Mbosso amenilipa pesa ndefu

Mbosso Sele Mj Selemani: Mbosso amenilipa pesa ndefu

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa maigizo Bongo ambaye amepata umaarufu kupitia Wimbo wa Mbosso wa Sele 'Selemani' amesema kuwa uongozi wa WCB umemlipa pesa ndefu ndiyo maana akakubali kufanya kichupa cha ngoma hiyo inayotikisa mjini kwa sasa.

Selemani ambaye anaishi mitaa ya Tandika amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya Mbosso kuachia video ya wimbo huo aliomshirikisha msanii Chley kutoka nchini Afrika Kusini.

"Kuna watu walioniunganisha mpaka nikafika pale, nikaona nichangamkie fursa. Nilipomuona Mbosso nikajisikia raha na burudani sana. Wamenilipa pesa nyingi sana kwenye ile video, wamenilipa vizuri na nimeridhika kabisa.

"Kwa sasa umri wangu ni miaka 25, sijafanikiwa kusoma niliishia darasa la saba kwa sababu ya hali ya kiuchumi ya familia yetu. Ninafanya Sanaa ya filamu na kujichanganya sokoni kutafuta chochote," amesema Sele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live