Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sele wa Mbosso: Nilivuta bangi nikataka kumpiga mama yangu

Selemani Mbosso Trs Sele wa Mbosso: Nilivuta bangi nikataka kumpiga mama yangu

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa maigizo Bongo ambaye amepata umaarufu kupitia Wimbo wa Mbosso wa Sele 'Selemani' amesema kuwa maisha ya kuvuta bangi ameyapitia kama kijana lakini baadaye aliona ni kama yanampotezea mwelekeo wa maisha akaamua kuachana nayo.

Selemani ambaye anaishi mitaa ya Tandika amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya Mbosso kuachia video ya wimbo huo aliomshirikisha msanii Chley kutoka nchini Afrika Kusini.

"Mimi nimevuta bangi, maisha hayo nimeyapitia sana na sasa nimeshatoka kule. Nakumbuka niliwahi kuvuta siku moja, niliporudi nyumbani nikamkuta mama yangu namwambia ‘Bi mkubwa nioshee hiki kiatu.

"Mama akaona siko sawa lakini mimi nikamwambia niko sawa. Nilimkoromea sana, nilitaka kumkata vibao, akanionshea nikaingia ndani. Baada ya hapo nikaona hii itanipotezea njia, nikaachana nayo," amesema Sele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live