Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sean Paul asimulia Kolabo yake na Beyonce ilivyopatikana

Sean Paul X Beyoncee Sean Paul asimulia Kolabo yake na Beyonce ilivyopatikana

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Jamaica, Sean Paul, amefunguka ushirikiano wake na mwimbaji wa pop wa Marekani, Beyoncé ulivyoanzia mpaka ngoma yao ya ‘Baby Boy’ kuweka rekodi kote ulimwenguni.

Paul ameyasema hayo katika mahojiano yake na The Hollywood Reporter akidai kuwa Beyoncé alikuwa mwanga kwake baada ya kushirikiana kwenye kolabo ya wimbo wake wa ‘Baby Boy’ kutoka kwenye albamu yake ‘Dangerous Love’ iliyotoka mwaka 2003.

Aidha mwanamuziki huyo wa dancehall ambaye anaumri wa miaka 51 amedai kuwa wimbo huo ulifungua njia ya kukubalika kwa dancehall duniani na kuweka historia ya kufanya kazi na Beyoncé.

Hata hivyo Paul amesema kuwa aliwahi kufanya kazi na wasanii kama Busta Rhymes, Clipse, na Blu Cantrell, ambao walikuwa na mwelekeo wa hip-hop zaidi, lakini Beyoncé alionekana msanii mkubwa aliyekuwa akijaribu kitu kipya kwa kufanya kazi nayeye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live