Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sawae Lee akoshwa na 'Superstar' ya Diamond na Costa Titch

Costa Sawaelee Sawa Lee akoshwa na 'Superstar' ya Diamond na Costa Titch

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa maarufu Duniani kutoka nchini Marekani, Swae Lee ameonekana kukoshwa na ngoma ya supastaa wa Bongo Fleva, @diamondplatnumz aliyofanya na marehemu @costatitch wa Afrika Kusini iitwayo "Superstar".

Swae Lee ame-share video hiyo fupi wakati sakata lake la kushambuliwa na Wasauzi likiendelea ambapo alionekana kukazia tena suala hilo.

"Kuna watu wengi sana wametafsiri tofauti ujumbe wangu, lakini nataka niseme kwa watu wa kwanza kuanzisha Amapiano, salute kwenu, kuna kazi ipo njiani inakuja, eyooo!! You wanna be a Superstar," amesema Sawa Lee.

Diamond na Costa waliiachia ngoma hivyo miezi tisa iliyopita na mpaka sasa ina watazamaji zaidi ya milioni 12 kwenye mtandao maarufu wa YouTube.

Costa Titch alifariki dunia akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza mnamo Machi mwaka huu baada ya kuanguka alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha la Ultra huko Afrika Kusini katika kitongoji cha Johannesburg cha Nasrec.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live