Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sauti za Busara kurudisha heshima ya muziki (+Video)

1807 IMG 0125

Wed, 24 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Zikiwa zimebakia takribani wiki mbili kuelekea katika tamasha kubwa la muziki la Sauti za Busara litakalofanyika kisiwani Zanzibar ndani ya  Ngome Kongwe, Mji Mkongwe kisiwani Zanzibar, waandaji watamasha hilo wamewataka wadau kutumia fursa hiyo kwani Sauti za Busara ni brand kubwa.



Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahamoud amesema kuwa ” Ndani ya majukwaa matatu kwa siku nne, tamasha hili litakuwa na maonyesho 46 yenye hadhi ya kimataifa ambapo kwa asilimia 100 yatapigwa mubashar. Vilevile tamasha hilo litawaunganisha wasanii kutoka katika mataifa mbalimbali kama vile,Kenya, Uganda, USA, Denmark,Rwanda, Malawi, Zimbawe na kwingineko.”

Yusuf akaongeza ” Tamasha la Sauti za Busara linatoa kipaumbele kwa upande wa kiingilio ambapo mtu watalipa kiasi cha shilingi 10000 kwa siku moja ila kwa siku nne mtu huyo atalipa shilingi elfu ishirini, hii ni kwa Watanzania.”

“Kwa watu wa mjini Zanzibar ambao watashindwa kumudu kununua tiketi watapata fursa ya kuona burudani mubashara kila siku katika jukwaa lililopo katika bustani ya Forodhani, sherehe zitakazofanyika barabarani, matukio ya Busara Xtra na Gwaride la Carnival ambalo hufanyika kuashiria kuanza kwa tamasha hilo,” ameeleza Yusufu.



Baadhi ya vikundi vya Sanaa vitakavyo pata nafasi ya kutumbuiza kwa upande wa Tanzania ni Msafiri Zawose, Jagwa Music, Leo Mkanyia, Tausi Women’s Taarab na Maulidi ya Homu ya Mtendeni

Chanzo: bongo5.com