Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Saudi Arabia kufungua Duka la Pombe baada ya miaka 70

Gashsc Saudi Arabia kufungua Duka la Pombe baada ya miaka 70

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saudi Arabia imesema itafungua duka la pombe kwa wahamiaji maalum wasio Waislamu, mjini Riyadh, likiwa la kwanza kufunguliwa kwa zaidi ya miaka 70.

Baadhi ya wateja wa duka hilo watakuwa wafanyakazi wa balozi, ambao kwa miaka mingi wameagiza pombe kutoka nje katika vifurushi na kuingizwa nchini humo kama mifuko ya kidiplomasia.

Marufuku ya kuuza pombe imekuwa sheria tangu 1952, baada ya mmoja wa watoto wa kiume wa Mfalme Abdulaziz ambaye alikuwa amekunywa hadi kulewa kumuua kwa kumpiga risasi mwanadiplomasia wa Uingereza.

Duka hilo jipya litakuwa katika eneo linalopendwa sana na wanadiplomasia katikati ya jiji ambapo masharti yake ni kwamba wanywaji watatakiwa kujiandikisha kabla na kupokea kibali kutoka kwa serikalini

Aidha wenye umri chini ya miaka 21 hawataruhusiwa dukani huku Mnywaji akitakiwa kwenda kununua mwenyewe na sio kutuma mtu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live