Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saraphina afunguka kusainiwa na Harmonize

Phina (Saraphina) Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Sarahina

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Sarahina ametolea ufafanuzi zile stori za kuhusishwa na kusainiwa katika label ya Konde Gang ya msanii Harmonize ambapo ameeleza kuwa hakuna ukweli wowote kuhusiana na hilo na kuongeza kuwa yeye yupo sawa bila kuwa chini ya lebo yoyote.

Kupitia wasafi fm Phina amesema; "Kuhusu kusainiwa Konde Gang sio kweli sijawahi kusainiwa wala kutaka kusainiwa na Konde Gang hajiwahi kutokea kabisa, Harmonize tumewahi kuwasiliana yes kwasababu kipindi imetoka Upo Nyonyo yeye na Kajala walikuwa wananisapoti sana muziki wangu so tukawa na project tunafanyia kazi.

"So nafkiri labda uo ukaribu wakati nina project na Harmonize nafkiri watu wengi wametafsiri tofauti, ujue watu wana matamanio yao huku nje wanatamani kwasababu Phina ni msanii ambaye hayupo kwenye label yoyote si angeingia na yeye kwenye label mambo yabadilike kidogo lakini mimi niko sawa,'' amesema Phina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live