Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sania wa Masogange amshukuru Uwoya

Sania Na Uwoya Sania wa Masogange amshukuru Uwoya

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto pekeee wa marehemu Agness Masogange, Sania Sabri amemshukuru muigizaji Irene Uwoya kwa kuendelea kumpa msaada mbalimbali katika masomo yake.

Sambamba na Uwoya, Sania amewashukuru pia mastaa mbalimbali pamoja na ndugu zake ambao awanaendelea kumlea vizuri na sasa anaelekea kumaliza kidato cha nne.

“Wengi tu wananisaidia vifaa vya shule kama madaftari na vitu vingine. Namshukuru Uwoya na ilikuwa tuonane lakini ilishindikana lakini ananisaidia sana,” alisema Sania.

Masogange aliyekuwa akitikisa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata alifariki dunia Aprili 20, 2018 katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar alikolazwa kwa siku nne akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia (Nimonia).

Mwili wake ulipumzishwa kijijini kwao Utengule jijini Mbeya baada ya kuagwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

Mrembo huyo aliyeonekana kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva kama Masogange ya Belle 9, Msambinungwa ya Tundaman na nyinginezo ameacha mtoto huyo mmoja pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live