Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia mgeni rasmi Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Songea

Samia Mgeni Rasmi Tamasha La Utamaduni Songea.png Samia mgeni rasmi Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Songea

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha tamasha la tatu la utamaduni la kitaifa litakalofanyika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Katika tamasha hilo, kutafanyika mdahalo wa kitaifa kuhusu mapambano dhidi ya viashiria vya mmomonyoko wa maadili.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 10, 2024, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema tamasha hilo litafanyika kuanzia Septemba 20 hadi 23, 2024.

Amesema tamasha hilo litafunguliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro na mgeni rasmi atakuwa ni Rais Samia.

Msigwa amesema tamasha hilo limetanguliwa na matamasha mengine ya kitaifa yaliofanyika jijini Dar es Salaam mwaka 2022 na lililofanyika Mkoa wa Njombe mwaka jana.

“Matamasha yaliyotangulia yamehusisha maonyesho ya bidhaa za kitamaduni na uuzaji wa bidhaa za wajasiriamali, bendi za muziki, maigizo, taarabu, maandamano, fani za jukwaani sanaa za ufundi, machapisho na vitabu, tiba za asili na vipodozi, ubunifu wa mitindo na ulimbwende, midahalo, vyakula vya asili, michezo ya jadi na utangazaji wa utalii,”amesema.

Ametaja baadhi ya mambo yatakayokuwa katika tamasha la mwaka huu, kuwa ni mirindimo ya kiasili, kuanzia mavazi, maonesho, visasili (ngoma na tafsiri) na visakale (mambo yanayosadikika) ambavyo vijana waliozaliwa mwaka 2,000 hawajawahi kusikia.

Msigwa amesema tamasha litakuwa na onesho maalumu la matumizi ya kanga ikiwa ni vazi la utamaduni wa Mtanzania, ushiriki wa zaidi ya vikundi 25 kutoka Tanzania bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live