Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia awashukuru wasanii waliotunga nyimbo kumuomboleza Magufuli

Wasanii Pic Data Samia awashukuru wasanii waliotunga nyimbo kumuomboleza Magufuli

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewashukuru wasanii waliotunga nyimbo mbali kwa ajili ya kuomboleza msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, John Magufuli.

Rais Samia ametoa shukurani hizo leo, Ijumaa Machi 19, 2021, Ikulu Dar es Salaam, alipokuwa akiapioshwa kuwa Rais.

Samia amechukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika hotuba yake ya kulihutubia taifa mara baada ya uapisho huo alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo ratiba ya mazishi.



Related Walichosema mastaa wa kike baada ya Samia Suluhu kuapishwa kuwa RaisPia alitumia fursa hiyo kutoa shukurani zake kwa namna mbalimbali watu walivyoshiriki katika msiba huo mzito tangu siku ya kwanza alipoutangaza, huku akiwagusa na wasanii waliotunga nyimbo kwa ajili ya maombolezo.

Mpaka sasa wasanii ambao wametoa nyimbo hizo za maombolezo ni pamoja na Harmonize, Rayvanny,, Christina Shusho,Peter Msechu, Kala Jerimiah na wengine bado wako studio wakiendelea kupika nyimbo hizo.
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz