Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia atoa neno kwa wasanii, wachezaji

403ff46685c64ea6b5545964cbd050dd.jpeg Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Sat, 1 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza wanamichezo na wasanii kwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali katika mwaka uliopita wa 2021.

Samia aliyasema hayo katika hotuba yake kwa wananchi ya kuuaga mwaka 2021 na kukaribisha mwaka 2022.

Akizungumzia Sanaa, Michezo na Utamaduni, alisema tunajivunia vijana wetu kwa upande huo, ambapo timu ya taifa ya soka ya walemavu (Tembo Warriors) imefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Uturuki Oktoba mwaka huu, Tembo Warriors ni miongoni mwa timu nne zinazowakilisha Afrika katika Kombe la Dunia baada ya kufanya vizuri katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika yaliyofanyika nchini hivi karibuni.

Pia Samia aliipongeza timu ya taifa ya soka la wanawake kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzanite, ambayo nayo imekaribia kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Costa Rica.

“Tunawapongeza kwa kubakiza hatua moja ya kushiriki Kombe la Dunia kule nchini Costa Rica na Mungu awasaidie wapate sifa ya kwenda huko, “alisema wakati wa hutuba hiyo.

Aliwapongeza Warembo na Watanashati wetu viziwi, ambao watashiriki Mashindano ya Dunia kule Brazil.

“Haya ni mafanikio makubwa kwetu katika medani ya michezo. Ni fahari kwetu pia kuona vijana wetu wa tasnia ya muziki wameshiriki na kupata tuzo mbalimbali katika ngazi za kimataifa. Kwa ujumla tumeshuhudia ukuaji katika sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live