Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

‘Samahani mpenzi’ zikizidi, huyo hakufai!

Couple Had Fight ‘Samahani mpenzi’ zikizidi, huyo hakufai!

Tue, 8 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SI UNAJUA bila mapenzi hakuna maisha! Huo ndiyo ukweli, huwezi kuishi kama jiwe au mti. Raha ya maisha ni kuwa na mpenzi wa kumpenda na yeye akakupenda kiukweli na siyo kuigiza kama ilivyo kwa baadhi ya watu.

Kwa wale walio katika mapenzi matamu na ya kweli watakubaliana na mimi kuwa mapenzi yenye amani na masikilizano ni kama ‘kapepo’ kadogo ndani ya ulimwengu huu mkubwa uliojaa vituko!

Kuna watu ni wagumu sana kuomba msamaha. Yaani wanajua wamekosa lakini wanaona kuomba msamaha ni kujishusha. Hii ni mbaya sana na inaweza kusababisha kupunguza mapenzi kati ya wawili waliotokea kupendana.

Pia kuna ambao ni wagumu kusamehe. Yaani mpenzi wake kafanya kosa kwa bahati mbaya na anagundua amekosea lakini akiomba msamaha, hasamehewi. Hili nalo ni tatizo!

Ila sasa kuna watu ambao kila siku ni samahani tu. Wapo ambao kila siku wanakosewa na wapenzi wao na kuishia kuombwa msamaha. Hili kimsingi ni jambo linaloweza kuleta picha ya tofauti.

Tunachojua ni kwamba, unafanya kosa leo, unaomba msamaha na kutorudia tena kosa. Lakini kama leo unamsaliti mwenzako, anakusamahe, kesho tena unasaliti, kwa kuwa anakupenda anakusamehe, keshokutwa tena unarudia kosa lilelile, katika mazingira hayo ni kweli unastahili kuendelea kusamehe?

Lakini kama mpenzi wako atakukosea makosa mawili-matatu kisha ukafanya maamuzi ya kumuacha, utakuwa unadhihirisha kwamba, hukuwa na mapenzi ya dhati kwake na ndiyo maana kakukosea mara moja au mbili, ukaona ndiyo mwanya wa kumpiga kibuti. Tujenge utamaduni kwa kusameheana kwani hakuna aliyekamilika kwa asilimia 100 na ndiyo maana kila siku tunakoseana.

Lakini kama kila siku wewe umekuwa wa kumkosea tu mwenzio na kuomba msamaha, unasamehewa hilo ni tatizo na hata neno msamaha lenyewe linakuwa halina maana kwako na kwa mpenzi wako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live