Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sallam na kiki za maradhi mbalimbali

102172 Pic+alam Sallam na kiki za maradhi mbalimbali

Sat, 11 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam Sharaf amesema kuwa hawezi kufanya kazi na msanii anayetafuta kiki ya ugonjwa.

Alisema msanii atakayefanya hivyo atakuwa ni mtovu wa nidhamu kwa Mungu.

Sallam ambaye ni miongoni mwa Watanzania waliougua corona hali iliyoibua maswali huku baadhi ya watu wakidai kuwa alikuwa anatafuta kiki jambo ambalo amelikana kwa nguvu zote.

“Nafahamu mara ya kwanza nilivyoweka wazi kuhusu kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa corona, watu walihusisha na kiki,” alisema Sallam katika mahojiano na mtandao wa Dizzim online .

Alisema ndiyo maana alipobainika ana corona alijali kwanza afya za wengine.

Alifafanua kitu cha kwanza alichofikiria baada ya kugundulika ni kuhakikisha watu aliombatana nao kwenye safari wanafuatiliwa na jamii inaondoa taharuki ambayo ilianza kujengeka.

Pia Soma

Advertisement
“Maneno yalishaanza kuzungumzwa kwenye mitandao ya kijamii nikaona kuondoa hiyo ni bora niweke wazi mwenyewe ili kuepusha taarifa za uongo zisizidi kusambaa na kusababisha taharuki ndiyo maana nikaweka wazi baada ya kuona kuna vitu vingi kwenye jamii bado havijaeleweka,” alisema.

Alisema licha ya kuwa alijihisi mapema kwamba huenda amepata maambukizi ya ugonjwa huo na kuwaeleza wenziy aliokuwa nao ili

wachukue tahadhari ila bado hakuwa na uhakika kama wanaweza kuwa salama.

“Nilimwambia daktari aniambie ukweli kuhusu majibu kama nina maambukizi ili tuone namna ya kuwasaidia wenzangu. Hatimaye akaniambia na mimi nikawaambia wote niliokuwa nao kuhusu hali yangu ili wawe kwenye uangalizi.

“Mawasiliano yalifanyika na yakatolewa maelekezo wakae kwenye karantini, wapo waliotaka kubisha kwa madai kuwa wako safi, nikalazimika kutumia vitisho kama kiongozi ndipo walipoanza kutaja watu waliokutana nao baada ya kurejea nchini. Wakaanza kufuatiliwa na wao hatimaye wakakaa karantini kwa siku 14, wamepimwa wote hakuna aliyekutwa na corona,”.

Sallam anasema licha ya kuwa taarifa za ugonjwa wake ziliwashtua wengi lakini Diamond alionekana kuwa mwenye wasiwasi zaidi na alikuwa akifuata maelekezo ya kila alichomwambia.

Akifafanua lisema, “Diamond aliposikia niko positive alikuwa na wasiwasi kupitiliza na alichukulia suala hili kwa uzito mkubwa. Nikimpigia tu simu kitu cha kwanza ananiambia ‘napiga machungwa hadi 15 kwa siku’.

Chanzo: mwananchi.co.tz