Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sallam afungua kituo cha radio

IMG 20221217 WA0003 Sallam Sallam afungua kituo cha radio

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbali na kwamba tuliona Diamond Platnumz na Majizzo kuingia headline za umiliki wa vituo vya Radio vya urushaji wa Matangazo nchini.

Sasa Meneja Sallam Sk nae hakusubiri mwaka huu uishe bali nae anamiliki kituo kipya cha Radio kiitwacho Mjini Fm ambacho Frequency zake ni 92.5 fm kama ukiwa Dar es Salaam ama Zanzibar utaisikia kwa umakini kabisa.

Kituo hicho kina miezi kadhaa tangu kianze kurusha matangazo yake na miongoni mwa  watangazaji waliopewa dhamana ya kutangaza katika kituo hicho ni Jimmy Kabwe, Abby Plaatjes, Soggy Dogg, Binah Kasembo na wengineo.

Akizungumza na Millardayo.com Mkurugenzi wa kituo hicho Sallam Sk alisema..”Imekuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu na ukimya wangu umetoa majibu kwamba hiki ndicho nilikuwa nakimpambania usiku na mchana si kitu rahisi sana lakini mpaka kufikia hapa nilipo ni hatua kubwa napenda kumshukuru Mungu sana”– Sallam SK

“Na nimeingia katika Challenge ambayo sio ndogo katika upambanaji bali ni kubwa sana unajua kumfanya mpaka msikilizaji asikilize Radio yako si kitu rahisi inategemea wewe umeandaa kitu gani kitakachomfanya asikilize kimvutie kwahiyo kuna vitu vingi vipya vinakuja wapenzi wa Radio watengee sikio 92.5 ndio Frequency yetu  masafa yapo mpaka Zanzibar hata ukiwa Dsm unatupata’- Sallam SK

Pichani Mkurugenzi wa 92.5 MjiniFm Sallam Sk  akiwa na Balozi wa Ufaransa Mhe, Nabil Hajlaoui, alipotembelea ofisi zao kwaajili ya mahojiano maalum kwenye kipindi cha Big City Breakfast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live