Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sallam SK ampongeza Rais Samia

Afe Sallam Sk Sallam SK ampongeza Rais Samia

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Sallam SK ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutokana na Uongozi wake pamoja na makubwa anayofanya.

"MY PRESIDENT DR. SAMIA SULUHU HASSAN. Pongezi kwa kiongozi wangu wa Nchi kwa misimamo yenye manufaa na nchi na kutoyumbishwa na wachache wenye mitazamo kwa ajili ya maslahi yao binafsi, ifike mahala tujue thamani ya nchi yetu na tunachokidai, nimebahatika kutembea nchi nyingi za Africa, kuna taifa kubwa na wote tunalijua umeme kwa siku ni masaa matatu tu.

Kuna nchi miundombinu yao ya barabara huwezi kwenda mkoa mwingine bila ndege leo hii Tanzania kila mkoa umeonganishwa na lami, nadhani ifike wakati watu waache kujimilikisha sauti za Watanzania wote kusema “ETI WATANZANIA WANATAKA KATIBA MPYA” Mimi nataka Maendeleo ya Nchi tufanye kazi kwa amani tupate kipato tusaidie familia zetu, na ndicho nachoona Rais wangu anachokifanya kwa sasa kwenye maendeleo ya nchi.

Ukirudi swala la Bandari nimefanya kazi ya Clearing and Forwarding miaka 5 na najua nje ndani matatizo ya bandari na nia ya serikali kuboresha kwenye bandari. Wengi wapiga kelele ni wakwepaji kodi ifike mahali tukubaliane na ukweli, kelele zinazoendelea ni bora tungemuomba kiongozi wetu wa nchi aangalie uwezekano wakupunguza baadhi ya vitu kodi ili tuweze kuendelea kunufaika na utawala wake bora.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUNGU MBARIKI RAIS WANGU ????????"---@sallam_sk .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live