Mwanadada nguli kwenye sekta ya Utangazaji Tanzania, Salama Jabir amesema kuwa yeye hasikilizi vituovya radio vya Tanzania kutokana na radio hizo kupoteza mvuto wa kimaudhi.
Salama Jabir amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari huku akidai kuwa radio za Bongo zimebaki kusifia badala ya kufanya kazi zake za kuuhabarisha umma, kuelemisha na kuburudisha.
"Mimi ni Mtangazaji lakini nisiwe mnafiki sisikilizagi radio za Tanzania, sisikilizi kwasababu radio za sasa hivi zimepoteza mvuto zimetoka kwenye lengo la kuhabarisha.
"Zimebaki za kulipizana kisasi tu mtu anaenda kumwaga pesa kwenye kitua cha radio ili kimsifie, au anatoa pesa kwa Mtangazaji ili amchambe mtu fulani, au nyimbo za fulani zisipigwe.
"Kwahiyo ukisikiliza radio za sasa hivi zimejaa kusifia tu hata kisichosifika, wakati huko mtaani kuna mambo mengi ya kuongelewa ambayo ndiyo yanapaswa kusika kwenye radio, kwahiyo mtanisamehe mimi sisikilizi hizi radio zenu mpaka mtakapobadilika"- amesema Salama Jabir.