Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la wanaume kuzuiwa kusuka Zanzibar, AT amlilia Rais Mwinyi

Msanii At Rs Sakata la wanaume kuzuiwa kusuka Zanzibar, AT amlilia Rais Mwinyi

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa muziki wa duara Visiwni Zanzibar, AT ameibuka na kumshauri Rais wa Zanzibar, Ally Hassan Mwinyi kuzuia wanaume waliosuka nywele zao.

AT amesema hayo ikiwa ni siku moja tangu mamlaka nchini humo zilipotangaza sheria kuwa wanaume waliosuka nywele hawaruhusiwi kukanyaga visiwani humo na endapo atataka kusuka basi atalazimika kupata kibali ambacho gharama yake ni Tsh milioni 1.

“Mimi nimeposti na watu wameona, hata serikalini kuna viongozi wamenipigia simu wakisema niko sawa, na wasanii wenzangu wamesema niko sawa.

“Baba yangu mzazi tangu azaliwe ana zaidi ya miaka 50 hajawahi kusikia hilo suala, hata wananchi wa Zanzibar hawajawahi kusikia hilo suala, yeye mwenyewe ameshangaa.

“Jambo hili ni kama limekuja kuleta taharuki, lakini ninaimani Rais Mwinyi amesikia na ni msikivu, ataona namna ambavyo atafanya acha tuvumilie tusubiri tuone.

“Kwa sisi Wazanzibari kufanyiwa hivi haina shida lakini tatizo lipo kwa wenzetu wageni, wengine ni watalii, itasababisha tuzungumzwe vibaya. Jambo kama hilo walitakiwa walizungumze mapema waweke taratibu mitandaoni watu wajue wakija Zanzibar kuna hiki na hiki.

“Bado tunaweza kubadilisha vipengele ambavyo vimewekwa kwa sababu katiba sio msaafu, unaweza kubadilisha muda wowote kwa sababu hata katiba tumebadilisha mara nyingi tu.

“Kuna tofauti kubwa kati ya dini, sanaa, mila na utamaduni, kama tumekubali kuwa na Wizara ya Sanaa hata kusuka ni Sanaa unasanifu nywele, kama lugha leo tuna maneno kama ‘maokoto’ yanaingia na kutoka.

“Ukishaingiza tu Sanaa ujue watu watafanya usanifu, nadhani tusubiri tuone Rais atakachofanya lakini kwa upande wangu nadhani nimeshatoa kile ambacho Rais anapaswa kuambiwa na watu wanasubiria juu ya hilo tu,” amesema AT.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live