Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la mkanda wa ngono, Ray J ailipua tena familia ya Kim Kardashian

Kim Ray J.jpeg Sakata la mkanda wa ngono, Ray J ailipua tena familia ya Kim Kardashian

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ray J(41) amlipua mama yake Kim Kardashian, Kris Jenner(66) kwamba ndie aliyesuka mpango mzima kwa mkataba ili kuvujishwa mkanda wake wa ngono na binti yake huyo mwaka 2007.

Hiyo tisa, kumi Ray J ameenda ndani zaidi kusema kuwa Mama yake Kim aliwahimiza warudie kuushuti mkanda karibia mara tatu ili binti yake aonekane katika angle nzuri zaidi.

Katika kipindi kipya cha The Kardashian kupitia Hulu, familia hiyo ilionekana kujadili tena suala la mkanda huo kitu ambacho kimeonekana kumtibua waziwazi Ray J hivyo kuibuka kusema mara zote familia hiyo inamuongelea katika namna aonekane yeye Ray J ndie aliuvujisha na hata katika interview mpya mama yake Kim alipoulizwa alikataa kumsaidia binti yake kuachia mkanda husika na kudai hasemi uongo.

Ray J ameeleza mama yake Kim ndie alisaidia wao wasaini mkataba kupitia kampuni ya Vivid na baadaye Ray J na Kim Kardashian(41) wakajulishwa kwa email kuwa mkanda husika umeingiza pesa zaidi ya dola milioni $1 mwaka 2007 mauzo zaidi yakitoka katika DVDs kisha Ray J na Kim kugaiwa faida ya mauzo kila mmoja.

Ray J ameonesha sehemu ya ushahidi wa mkataba, mwandiko wa Kim na email walizotumiwa mwaka 2007 yeye na Kim toka kampuni husika.

Ray J na Kim walianza kuwa wapenzi 2003 hadi 2006 kipindi ambapo Ray J ndie star Kim akiwa hana umaarufu wowote. Lakini kuvujishwa kwa mkanda husika wa ngono ndio hasa ikawa tiketi ya Kim Kardashian kutupwa katika ulimwengu wa umaarufu ghafla na sasa kawa Bilionea.

Baada ya Ray J kusema Kris Jenner ndie alimsaidia mwanae mkanda uvujishwe, Kim Kardashian na Mama yake bado kuzungumza kujibu alichosema Ray J ambaye amesema amechoka kuvumilia na kuonekana mbaya siku zote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live