Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Mtoto Kuunganishwa TikTok, Kim Amjibu Kanye

Kim Kanye Sakata la Mtoto Kuunganishwa TikTok, Kim Amjibu Kanye

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda mfupi baada ya rapa Kanye West kuonesha kutoridhishwa kwake na mwenendo wa jinsi mzazi mwenzie anavyomlea mtoto wao North West,  hatimaye Kim Kardashiani ameshindwa kuvumilia na kuamua kufunguka kuhusu suala hilo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) Kim amesema kuwa  "mashambulizi ya mara kwa mara" kutoka kwa Kanye kwenye mahojiano na kwenye mitandao ya kijamii yamekuwa ya kuumiza zaidi kuliko yeye alivyoumizwa na TikTok ya North West ."

"Kama mzazi ambaye ndiye mlezi mkuu wa watoto wetu, ninafanya kila niwezalo kumlinda binti yetu huku pia nikimruhusu kuonesha kiwango cha ubunifu wake,” aliandika Kardashian na kuongeza kwa kusema kuwa.

“Talaka ni ngumu vya kutosha kwa watoto wetu mimi na Kanye. hamu ya kujaribu kudhibiti na kuendesha hali yetu vibaya na hadharani inasababisha maumivu zaidi kwa wote, sihitaji chochote ila uhusiano mzuri na wenye kutuunganisha kama wazazi wenza."  Aliandika Kim Kardashian.

Hii ni mara ya kwanza kwa siku za hivi karibuni  Kim kumjibu Kanye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live