Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Harmonize, Jeshi la Polisi limetoa tamko kwa mara ya kwanza

Screen Shot 2021 04 20 At 3.46.44 PM 660x400.png Sakata la Harmonize, Jeshi la Polisi limetoa tamko kwa mara ya kwanza

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa picha za utupu zikimuhusisha Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rajab Abdul Kahal maarufu kama Harmonize.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hadi sasa wamehojiwa Watu watano kuhusiana na sakata hilo na wapo nje kwa dhamana.

“Watuhumiwa hao ni Frida Kajala Masanja (36), Paula Paul Peter (18), Raymond Mwakyusa maarufu RayVanny (27), Claiton Revocuts maarufu Baba Levo (34), Catherine John na Juma haji (32)”-MAMBOSASA

“Watuhumiwa hawa wote walikamatwa, wakahojiwa na kwa vile dhamana ipo wazi wapo nje kwa dhamana na taratibu za upelelezi zinaendelea zikikamilika jalada litaenda kwa Wakili Mkuu wa Serikali na kama akiona kuna jinai watafikishwa Mahakamani”-

Chanzo: millardayo.com