Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Saitoty mwenye miaka 30 afunga ndoa na bibi mzungu wa miaka 60

Saitoty D.jpeg Kijana wa Kimasai wa miaka 30 afunga ndoa na mzungu wa miaka 60

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamama Deborah (60) ambaye ni afisa mstaafu wa jeshi la polisi nchini Marekani ameolewa na kijana wa Kimasai kutoka Tanzania kwa jina la Saitoty Babu (30)

Akielezea, Deborah amesema mwaka 2017 aliingia Zanzibar yeye na binti yake anayefahamika kwa jina la Royce (30) ndipo wakiwa ufukweni wakaona vijana wawili wa Kimasai mmojawapo akiwa ni huyo Saitoty.

Kwa sababu katika maisha yake hakuwahi kukutana na mtu wa jamii ya Kimasai hasa aliyevaa Kimasai, Debora aliomba kupiga nao picha kama ukumbusho, baadaye Saitoty aliomba atumiwe hiyo picha na ndipo akayapata mawasilianao ya Deborah wakaanza kuwasiliana.

Deborah alirudi kwao Califonia nchini Marekani lakini Saitoty akawa anawasiliana nae na kumgusia kuwa anataka kumuoa Deborah.

Wawili hao wanasema kutofautiana umri kwa miaka 30 halikuwa jambo baya kwao na huba hilo lilichagizwa na mama huyo kuwa singo (hakuwa na mume) lakini alikuwa anaishi kwa furaha. Ilichukua takribani miezi mitano tu, Deborah alikuja kutalii tena Tanzania wakaonana tena.

Wameeleza kuwa, siku moja Deborah akiwa akiwasiliana na Saitoty kwa FaceTime, akamuonesha kwa watoto wake wengine wawili, wa kike Tiffany (32) na wa kiume Sherrick (27) ambao hawakuwa na hiana mama yao kuolewa na Saitoty.

Watoto walimueleza mama yao kuwa umri sio kigezo kama kakupenda na unaona mkiwa pamoja utakuwa na furaha basi sio mbaya kuolewa nae.

Wawili hao walifunga ndoa ya kimila nchini Tanzania mwaka 2018 na mwaka huu 2022 ndipo wamefunga ndoa ya kiserikali ila Deborah bado ana matumaini watafanya sherehe kubwa kwa mujibu wa mila za kimasai ili familia zote mbili zijumuike.

Tayari Deborah amepewa jina la Kimasai anaitwa Nashipai na ameanza kutumia jina la mume wake huyo yaani Deborah Nashipai Babu

Baada ya kufunga ndoa, Debora amehamia Tanzania na wanaishi katika nyumba ya udongo (boma) na mume wake huyo maeneo ya Ubena.

Deborah amesema maisha ya Marekani na Tanzania yanatofautiana sana ila bado anafurahia kuishi Tanzania licha ya kwamba kwasasa anapikia kwa kutumia kuni na maji walipo ni shida kidogo. Pia eneo wanaloishi kwasasa wanajenga Lodge.

Changamoto ya penzi lao amesema ni watu baki au wananzengo kuwakalia kooni kwa kusema Saitoty amemuoa Deborah ili apate uhalali wa kwenda kuishi Marekani(green card) lakini Deborah amepangua kwa kusema mume wake huyo hata hana hamu kivile ya kwenda kuishi Marekani.

Pia, Debora amesema watu wengine wanamnanga kwa kumkejeli kuwa Saitoty ni mjukuu wake na wengine wakimwambia amemuasili(adopt) Saitoty.

Ila amesema familia zao wote zimewapa baraka na kamwe hakuwahi kudhani angekuja kuolewa na mwanaume aliyempita sana umri ila wanapendana sana wote ni wacheshi na wote wapo romantic bila kusahau Saitoty hufanya chochote kile ili kumnunulia chocolate Deborah.

Saitoty ambaye anachunga mifugo amesema pia mke wake huyo ni mtu muhimu katika maisha yake kwani anamsapoti katika mambo mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live