Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli ameweka bayani juu ya ujio wake mpya katika tamasha la muziki la Sauti za Busara kwa mwaka 2018.
Saida ambaye anatamba na vibao vyake matata ikiwemo, ‘Omulilo’,’Kichaka’ na ‘Maria Salome’ ambayo ilimuweka vyema katika uliomwengu wa muziki ameahidi kufanya vyema katika tamasha hilo.
“Nimefurahi sana kupata bahati ya kuperform Sauti za Busara kwa mara nyingine, Sauti za Busara nimeshawahi kwenda kushiriki mwaka 2005 na leo naenda kushiriki mwaka 2018. Ni miaka mingi na ndio maana wanasema nimepotea lakini nashukuru tena kunipokea na kunifanya ninyanyuke mara nyingine tena,” amesema msanii huyo.
Pia akasisitiza “Sauti za Busara ni sehemu nzuri ya kukutana na wenzetu na kubadilishana mawazo, kuonana na wenzetu tukabadilishana fikra na vilevile nyimbo zetu ni kwa ajili ya kuondoa mawazo kwenye vichwa vyetu.”
Tamasha la Sauti za Busara ufanyika kila mwaka mwezi wa pili, na hukutanisha wasanii tofauti tofauti katika muziki. Tamasha hili ufanyika kisiwani Zanzibar na limekuwa tamasha la kuvuta hisia za watu kwani muziki unakuwa Live.