Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sahau kuhusu Rayvanny: Khaligraph Jones kumuibukia Diamond?

7447 Khaligraph Diamond Bongo5 Pix

Fri, 4 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones amefunguka kuhusu mipango ya kufanya kolabo na Diamond Platnumz.



Hii ni baada ya kufanya kazi na Rayvanny ambapo walitoka ngoma inayokwenda kwa jina la Chalii ya Ghetto.

Rapprer huyo akipiga stori na JJ wa Jembe Fm amesema bado anaamini utafika wakati watafanya kazi ila hajaweka wazi iwapo wameshakaa na kuzungumza hilo.

“Diamond ni msanii ambaye ninamuheshimu sana, ametangaza muziki wake Afrika . Napenda kazi ambayo anafanya na ninaamini ukifika ule wakati wa sisi kufanya kazi pamoja tutafanya kazi nzuri, naamini itatokea hivi karibuni,” amesema.

Khaligraph Jones ameshafanya kolabo na wasanii wa Bongo kama Rosa Ree, Christian Bella, Chin Bees, Young Killer na Nikki Mbishi. Pia kolabo yake na Rostam (Roma na Stamina) ipo mbioni kutoka.

Loading...
Chanzo: bongo5.com