Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sahau kuhusu Dogo Janja na Gazza: Madee kukisanua tena kupitia MMB

7762 Qws TZW

Thu, 10 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo kutokea Tip Top Connection, Madee amesema hivi karibuni anatarajia kutambulisha msanii mpya kupitia brand yake ya Manzese Music Baby (MMB).



Madee amesema kutambulishwa kwa msanii huyo ni baada ya Dogo Janja na Gaza kufanya vizuri.

“Kuna Dogo Janja, kuna Gaza ambaye ameshatoa ngoma yake ya kwanza kabisa ilikuwa inaitwa Nanii na kuna mwingine mpya tutamtambulisha hivi karibuni anaitwa Dalla Day,” Madee ameiambia Bongo5.

Pia Madee ameeleza tofauti iliyopo kati ya Tip Top Connection na MMB, “Tip Top anaweza kuwa ni babu ambaye amemzaa mwanae MMB halafu watoto ndio watakuwa ndani,”.

Loading...
Chanzo: bongo5.com